WAZIRI UMMI AWATOA HOFU WANANCHI.
Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka wananchi waondoe hofu kuhusu tetesi za uwepo wa ugonjwa wa Uviko-19 huku akiahidi kutoa taarifa rasmi ndani ya wiki moja.
Ummy ameyasema hayo kupitia andiko lake katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram leo Mei 14, 2023.
Aidha, Ummy amesema takwimu za wagonjwa wapya wa Uviko-19 zinaonyesha wamepungua ikilinganishwa na kipindi kilichopita.
Pia, Ummy amesema hakuna kifo chochote kilicho thibitishwa kusababishwa na ugonjwa huo na amesema wizara ya Afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye hospitali mbalimbali na watatoa taarifa kamili.
Andiko hilo la Waziri Ummy linakuja baada ya tetesi za kurudi kwa ugonjwa huo nchini huku ukihusishwa na vifo mbalimbali vya watu maarufu vilivyotokea hivi karibuni.
No comments