BODI YA BIMA YA AMANA YAENDELEA NA MCHAKATO WA UFILISI.
Bodi ya Bima ya Amana imesema imo kaika hatua za ufilisi wa benki takriban tisa hapa nchini ambazo zimeonesha kushindwa kuendesha biashara zao za kifedha kwalengo la kuwarahisishia wananchi wanaotumia benk hizo kupata Amana zao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa bodi ya Bima ya Amana TANZANIA bwana Isack Kihwi wakati wa mafunzo maalum yaliyo andaliwa na benk hiyo kwa wahariri wa vyombo vya habari hapa Zanzibar yaliyo fanyika katika Ofisi za BOT zilizopo kinazini mjini ni unguja.
Akizitaja benki hizo ambazo zimeshindwa kuendesha biashara zake za kifedha nipamoja na Delphis,Greenland,,Covenant Benki for women,Meru Community Benki,Kagera Famers Cooperative benki,Njombe Community Benki,Elfatha Community Benki ltd,Mbinga Community Benki na FBME Benki.
Amesema kuwa mnamo mwezi February mwaka huu Serikali imeongeza kiwango cha juu cha kinga kwenye amana katika benki kutoka shilling 1.5 Million hadi Shilling 7.5 Million kama benki itakayo filisiwa.
Aidha mwenyekiti huyo amelitolea ufafanuzi suala la Benki ya FBME ambayo ilikuwa na ofisi zake hapa Zanzibar, amesema bodi ya bima ya amana ipo katika hatua za mwisho za kuwalipa stahiki zao wale wote waliokuwa wanamtumia benki hiyo.
Hata hivyo bwana kihwi anewaomba wateje waliokuwa wanamtumia benki hiyo kuwa wastahamilivu kwani serekali zote mbili zinalishuhulikia kwa umakini suala la benk ya FBME ili kuhakikisha wanufaika hao wanapata haki yao mara baada ya harakati za ufilisi wa benki hiyo kukamilika. See less
All reactions:
4
No comments