TUMBATU FM

Breaking News

WACHEZAJI ULAYA WAKUTANA NA UBAGUZI WA RANGI

 



BUKAYO Saka, nyota wa timu ya taifa ya England baada ya kukosa penalti kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Italia ya Euro 2020 amekuwa akiandamwa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii ambao wanaonyesha kila dalili za ubaguzi wa rangi.

Nyota huyo mwenye miaka 19 alitoka benchi na kupewa jukumu la kupiga penalti ya tano ambayo ilikuwa ni ya maamuzi Uwanja wa Wembley mwisho wa siku alikosa na kufanya Italia kuwa washindi wa pili baada ya Italia kushinda penalti 3 huku England ikishinda penalti 2.

Kipa wa timu ya taifa ya Italia Gianluigi Donnarumma aliokoa juhudi za Saka ambao walikuwa wanahitaji taji hilo kwa kuwa imepita miaka 55 bila kutwaa taji na mwisho wa siku wakalikosa pia.

Ripoti zimekuwa zikionyesha kuwa nyota huyo hana bahati kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Instagram ambapo jumbe nyingi zinazoonyesha viashiria vya ubaguzi wa rangi zimekuwa zikitumwa na kwenye akaunti yake pia amekuwa akikutana na meseji mbalimbali.

Bahati mbaya pia wengine wamekuwa wakituma emoji kwenye mitandao ya kijamii katika posti ambazo aliziweka muda mfupi kabla ya fainali huku mmoja wa watumiaji alisema kuwa "Ondoka katika nchi yangu na mwingine aliandika kwamba, "Nenda Nigeria".

Mbali na Saka pia Marcus Rashford pamoja na Jadon Sancho ambao walikosa penalti nao wamekutana na jambo hilo.

Shirikisho la Soka la Uingereza, FA imetoa taarifa kwamba itashughulia suala hilo kwa kuwa sio la kimichezo.


No comments