Ripoti ya Haki za Binadamu kutoka Kituo cha LHRC inaonyesha mauaji ya Wanawake kuuliwa na wenza wao kutokana na sababu mbalimbali yaliongezeka mwaka 2020 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Kulingana na ripoti hiyo, kwa mwaka 2020 yalikusanywa matukio 32 ya Vifo vya Wanawake waliouawa kwa sababu ya wivu wa mapenzi, wakati mwaka 2019 matukio ya aina hiyo yalikuwa 12

Pamoja na mauaji, zipo taarifa za wanaojeruhiwa hata kupata ulemavu kutokana na ugomvi ambao chanzo chake ni mapenzi. Pia, vitendo vya kujichukulia Sheria mkononi vinaendelea ambapo mwaka 2020 Watu 443 waliuawa na Watu wenye hasira pamoja na imani za kishirikina.