Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland
Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland

Manchester City inaamini ikiwa ni ichukue ubingwa wa Ligi ya Primia msimu huu ni lazima iipiku Chelsea katika usajili wa mshambuliaji wa Borussia Dormund raia wa Norway Erling Braut Haaland, 20. (Star)

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema huenda mshambuliaji wa Ufaransa Paul Pogba, 27, akafikia makubalino mapya na Old Trafford. (Guardian)

Reds imekamilisha usajili wa kiungo wa kati anayesemekana kuwa na thamani ya juu Kaide Gordon, 16, kutoka Derby County. (Mail)

Mohamed Salah
Maelezo ya picha,

Mohamed Salah raia wa Misri

Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 28, huenda akawa mchezaji atakayeondoka ikiwa Liverpool itafikia makubaliano na mshambuliaji wa Paris St-Germain raia wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, msimu huu. (Marca)

Chelsea itajitahidi kuishinda Real Madrid katika usajili wa mlinzi wa Bayern Munich raia wa Austria David Alaba, 28, ambaye ataondoka timu ya mabingwa wa Ujerumani mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu. (Guardian)

Dayot Upamecano
Maelezo ya picha,

Dayot Upamecano

Wakati huo huo, matumaini ya Chelsea ya kusajili walinzi wawili waliokuwa wamewapa kipaumbele -mchezaji wa kimataifa wa RB Leipzig raia wa Ufaransa Dayot Upamecano, 22, na Niklas Sule, 25 wa Bayern Munich raia wa Ujerumani - sasa kutategemea sana mipango ya uhamishi ya Bayern. (Goal)

Blues badala yake huenda ikaanza kunyatia mlinzi wa Bayern raia wa Ujerumani Jerome Boateng, 32. (Bild - in German)

Jesse Lingard,
Maelezo ya picha,

Jesse Lingard

West Ham haitakimbilia kufanya maamuzi ya kubadilisha mkataba wa kiungo wa kati England Jesse Lingard kutoka Manchester United ambaye yuko kwa mkopo kuwa wakudumu. (Standard)

Leicester City inafanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 23, juu ya mkataba mpya wa pauni 100,000 kwa wiki. (Mail)

Kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard, 22, kuna uwezekano mkubwa akafikia makubaliano ya kudumu na Arsenal ikiwa Zinedine Zidane atasalia kuwa kocha wa Real Madrid. (Eurosport)

Martin Odegaard, amewsiliana na Arsenal
Maelezo ya picha,

Martin Odegaard huenda akahamia Arsenal

Kocha wa Real Zidane anasema kuwa alimsihi Odegaard kusalia kwenye klabu hiyo kwa muda wa nusu ya msimu. (Metro)

Aliyekuwa winga wa Arsenal Marc Overmars anataka kurejea kwenye klabu hiyo kama mkurugenzi wa soka. Sasa hivi anashikilia wadhifa huo huo Ajax. (De Telegraaf, in Dutch)

Manchester United haina tena tamaa sana ya kumsajili beki wa kati mpya kwasababu ya mlinzi wao Harry Maguire. (Manchester Evening News)

Max Aarons
Maelezo ya picha,

Max Aarons

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer yuko makini kumsajili beki wa kulia Max Aarons, 21, kutoka Norwich City dirisha la usajili litakapofunguliwa tena. (Express)

Wakati huo huo, Solskjaer huenda akakabiliwa na ushindani mkali katika usajili wa Aarons kutoka Tottenham, huku Spurs ikimnyatia mlinzi huyo kama mwenye uwezekano mkubwa wa kuwa mbadala wa beki wa kulia kutoka Ivory Coast, Serge Aurier. (Eurosport)

Uwepo wa Gareth Bale, 31, Tottenham ambaye yuko huko kwa mkopo umeanza kutiliwa mashaka na uvumilivu juu ya mchezaji huyo kutoka Real Madrid umeanza kupungua kwasababu ya mchezo wake. (Mail)

Eden Hazard sitting on the pitch
Maelezo ya picha,

Eden Hazard

Chelsea ina nia ya kumsajili tena mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 30, kutoka Real Madrid msimu huu. (Defensa Central - in Spanish)

Kocha Jose Mourinho ana shinikizo Tottenham lakini hayuko katika hatari ya kupigwa kalamu. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Sheffield United John Lundstram anasema "kila kitu bado kiko wazi" kuhusu hatma yake, licha ya kuhusishwa na Newcastle United na Rangers. (Sheffield Star)

Lionel Messi
Maelezo ya picha,

Matumaini ya Paris St-Germain na Manchester City kumsaini Lionel Messi yafufuliwa

Mshambuliaji Lionel Messi, 33, hajafikia mkataba wowote na timu ya Paris St-Germain au Manchester City.

Mkataba wake na Barcelona ambao bado unasifika unamalizika msimu huu lakini atasubiri hadi mwisho wa msimu kuamua ikiwa atasalia kwenye klabu hiyo au atahamia kwengineko. (Goal)

Winga wa Ukraine Marian Shved, 23, amekubali kwamba alifanya makosa kujiunga na Celtic badala ya Genk miaka miwili iliyopita. Shved sasa hivi yuko kwa mkopo Mechelen kutoka Celtic. (Glasgow Live)

France's Kylian Mbappe
Maelezo ya picha,

Kylian Mbappe

Kylian Mbappe anataka kujiunga na Real Madrid, amesema Jese Rodriguez, aliyekuwa mchezaji mwenzake huko Paris St-Germain. (Marca)

Mlinzi wa Serbia Aleksandar Kolarov, 35, na beki raia wa Italia Matteo Darmian, 31, wote wanatarajiwa kuondoka Inter Milan msimu huu. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Vilabu sita vya Ligi ya Primia huenda vikacheza katika Ligi ya Mabingwa kuanzia mwaka 2024 kuendelea. Mapendekezo ya Uefa yatawezesha timu kucheza mechi 10 za makundi kila moja huku kukiwa na uwezekano Ligi ya Europa ikapunguza idadi ya timu zitazoshiriki ligi hiyo.

West Ham wanamtaka Mmrocco Youssef En-Nesyri
Maelezo ya picha,

West Ham wanamtaka Mmrocco Youssef En-Nesyri

West Ham inatarajiwa kutoa kitita kingine cha pesa kwa ajili ya mshambuliaji wa Sevilla raia wa Moroccan Youssef En-Nesyri, 23, msimu huu. (Star)

Timu kubwa za Ulaya zitapewa fursa ya kucheza katika Ligi ya Mabingwa hata kama zitashindwa kumaliza katika nafasi ya nne kwenye mashindano yao ya ndani, Uefa imesema hivyo kwa vilabu vya Ligi ya Primia kama moja ya mipango yake. (The Times - subscription only)