RONALDO SASA NI MTAMBO WA MABA0
CRISTIANO Ronaldo ndani ya Klabu amecheza jumla ya mechi 894 na ametupia mabao 674 akiwa ametengeneza jumla ya pasi 108.
Ndani ya La Liga rekodi zinaonyesha kwamba amecheza mechi nyingi ambazo ni 292 na alitupia jumla ya mabao 311 na pasi 96 akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dk 81.
Mtambo huo wa mabao katika Ligi Kuu England alicheza jumla ya mechi 196 na alitupia mabao 84 na pasi za mwisho alitoa 45 ambapo alikuwa na wastani wa kufunga kila baada ya dk 173.
Raia huyo wa Ureno mwenye miaka 36 kwa sasa anakipiga ndani ya Juventus inayoshiriki Serie A mkataba wake unatarajiwa kumeguka Juni 30,2022.
Ndani ya Serie A amecheza jumla ya mechi 97 alitupia mabao 81 na pasi za mwisho ni 17 akiwa na wastani wa kufunga bao kila baada ya dk 104.
No comments