Mgombea wa chama cha mapinduzi jimbo la Tumbatu kwa nafasi ya uakilishi Mhe Haji Omar Kher aanza na swala la kuhamasisha amani
Add caption |
Mgombea wa chama cha mapinduzi jimbo la Tumbatu kwa nafasi ya uakilishi Mhe Haji Omar Kher amewataka wananchi kudumisha amani kwa kuachana na vishawishi vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea campeni za uchaguzi
Akizungumza na radio jamii Tumbatu mara baada ya kurejesha fom ya uteuzi katika afisi ya tume ya uchaguzi iliyopo gamba mkoa wa kaskazini unguja amesema ili jamii iweze kuishi katika maisha bora hasa kwa kipindi hiki ni lazima kuzingatia swala la umuhimu wa amani
Amesema pamoja na kuwa mchakato wa uteuzi wa wagomea unasubiria maamuzi ya tume ya uchaguzi lakini ni vyema wagombea na wananchi wakachukua juhudi ya kudumisha ili kuiepusha nchi na machafuko
Kwa upande wa mgombea wa ubunge Mhe Juma Hija pamoja na mgombea udiwani Bw Makame Ali Chum wamewaomba wananchi kuendelea kuvuta subira na kufuatilia campen pale muda utapowadia
Wamesema pamoja na mambo mengi wanayotaka kuyaeleza kwa wananchi bado wanasubiri muda uliowekwa na Tume ufike ili waweze kutumia majukwaa kuyawasilisha kwa jamii
Na Makame Ngwali - Tumbatu FM
E/D Juma Hji .
No comments