Dkt Mwinyi kuchukua fomu kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi ccm visiwani zazibar
Dkt. Hussein Mwinyi aliyepitishwa kugombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo asubuhi anatarajia kuchukua fomu ya kugombea urais katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM (Zanzibar), Catherine Peter Nao amewaambia waandishi wa habari visiwani humo kuwa baada ya kuchukua fomu hizo katika ofisi ya ZEC, Dkt. Mwinyi ataungana na wanachama wa chama hicho katika Ofisi za Kisiwandui.
Akizungumzia hali ya uchaguzi wa mwaka huu, amewataka wanasiasa wote kuhakikisha wanafanya siasa za kistaarabu zinazozingatia hali ya usalama wa nchi.
Kiongozi huyo wa CCM amewasisitiza kuwa wana mgombea ambaye anakubalika kwa wananchi na anauzika kirahisi.
Akielezea matumaini yake kwa mgombea huyo amesema wanatarajia kushinda uchauguzi mkuu kwa asilimia 85 visiwani Zanzibar.
Na Zanzibar 24
E/D Juma Haji Juma- Tumbatu FM
No comments