TUMBATU FM

Breaking News

wazazi wenye watoto ambao hawajarudi shule warudi mara moja na kuendelea na masomo.



 

Afisa elimu mkoa wa kaskazini unguja Moh’d Mzee Chum amewataka wazazi wenye watoto ambao hawajarudi shule baada ya shule kufunguliwa kutikana na corona wahakikishe watoto wanarudi ili waweze kuendelea na masomo

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mahojiano maalum na kituo cha habari cha radio jamii Tumbatu katika mfululizo kazi zake za  kutoa elimu kwa wazazi na wanafuzi huhusu umuhimu wa elimu.

Amesema wizara bado inatoa nafasi kwa wanafuzi kurudi shule baada ya kukosa masomo kwa miezi miwili mfululizo kutokana na sababu ya ugonjwa au zuio la serekali.

Aidha amewataka walimu wakuu wa shule kuendelea kusimamia mashart ya afya ili kuhakikisha kazi ya ufundishaji inafanyika bila tatizo la aina yoyote.

Wakati huo huo baadhi ya wanafuzi wameipongeza serekali ya mapinduzi Zanzibar kwa kusogeza mbele mtihan ya taifa ili kuwapa nafasi wanafuzi kufidia muda walioupoteza kwa kipindi cha uwepo wa tatizo la corona

Mmoja kati ya wanafuzi hao kutoka shule ya secondary ya Tumbatu ambae hakutaka jina lake litajwe amesema hatua hii itaweza kurejesha matengemeo ya ufaulu kwa wanafuzi.

Na Rehema Makame – Tumbatu FM

E/D Juma Haji.

No comments