Wenyeviti wa mitaa watakiwa kuwapa elimu wanajamii kuhusu mvua
wenyeviti wa kamati za wilaya za kukabiliana na maafa wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuwaelimisha wananchi katika wilaya zao juu ya hatua stahiki wanazopaswa kuchukuwa kufuatia mvua za masika zinazotarajiwa kunyesha mwanzoni mwa wiki ya kwanza mwezi machi mwaka huu.
kaulli
hiyo imetolewa na shaabani seif mohamed mkurugenzi mtendaji wa kamisheni ya
kukabiliana na maafa zanzibar wakati
akizungumza na wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mabaraza manispaa offsin
kwake huko maruhubi katika kikao maalum
cha kujadilili muelekeo wa mvua za masika zinazotarajiwa kunyesha hivi
karibuni.
amesema
kuwa wenye viti wa mitaa wanawajibu wa kuelimisha jamii wanayoishi nayo juu ya mvua hizo ambazo zinaweza kuathiri
maisha ya watu na makazi yao.
aidha,
mkurugenzi huyo ameishauri jamii kuondokana na dhana kuwa suala la
kukabiliana na maafa ni la kamisheni pekee huku akisema kuwa taasisi mbali mbali na mtu mmoja mmoja
inafaaa kuchukua hatua stahiki katika
kuhakikisha tatizo la kutokea kwa maafa linapungua katika jamii wanazoishi.
akiwasilisha
mada ya mwelekeo wa mvua za masika afisa kitengo cha mawasiliano na tahadhari
za mapema kassim salum abdi amesema uzoefu unaonesha kuwa katika kipindi
cha mvua kubwa mkoa wa mjini magharibi
unaongoza kwa kukumbwa na athari ikiwemo mafuriko,maradhi ya kipindupindu
sambamba na kuziomba mamlaka husika kuchukua tahadhari ili kuepuka athari hizo.
nae
mkuu wa wilaya ya kaskazini “a” hassan
ali kombo amewaomba watendaji wa idara ya aridhi kuharakisha zoezi la upimaji
na ukataji wa viwanja ili kutoa fursa kwa wananchi kujenga katika maeneo rasmi
na kuepukana na tabia ya kujenga bila ya kuzingatia taratibu za mipango miji.
pamoja
na mambo mengine serikali imeombwa kulipatia ufumbuzi tatizo la kutuaama maji
katika eneo la fuoni kibonde mzungu ambapo uozefu unaonesha kila zinaponyesha
mvua kubwa husababisha athari na baadhi ya watu kupoteza maisha na mali zao.
No comments