Polisi nchini Uingereza wamesema takribani watu wanne wamefariki
Polisi nchini Uingereza wamesema takribani watu wanne wamefariki na wengine wanne kujeruhiwa kutokana na mlipuko uliotokea jijini Leceister lililoko katikati ya nchi hiyo.
Taarifa hiyo iliyotolewa na polisi wa eneo la Leceistershire, inaeleza kuwa watu wanne wanaendelea na matibabu hospitalini ambao mmoja kati yao alijeruhiwa vibaya, lakini mpaka sasa ni watu wanne waliothibitishwa kufariki.
Polisi hao pia wamesema idadi ya waliopoteza maisha inaweza kuongezeka kwa kuwa taarifa kamili ya uchunguzi haijakamilika.
Kikosi cha zimamoto kilitumia zaidi ya saa moja kuuzima moto uliotokana na mlipuko huo mkubwa.
Jana, jumapili jioni polisi hao wa Leceistershire, walisema mpaka sasa hakuna dalili zozote za kuhusisha mlipuko huo na tukio la ugaidi.
Mlipuko huo pia unadaiwa kuharibu duka moja na nyumba moja katika eneo hilo, huku wakazi wanaoishi kuzunguka eneo hilo wakisema walishuhudia mtikiso mkubwa kutokana na mlipuko huo.
No comments