Serikali ya Kenya inatarajia kupunguza ukopaji
Serikali ya Kenya inatarajia kupunguza ukopaji na uuzaji katika masoko ya hisa ya ndani kwa ajili ya matumizi makubwa na ya muda mrefu baada ya thibitisho la kupata mwitikio kutoka masoko ya hisa ya kimataifa yenye mitaji mikubwa.
Wiki iliyopita Kenya ilitangaza dhamana ya kimataifa, ya miaka 10 na ya miaka 30 kupitia mkupuo wa asilimia 7.3 na 8.3 ambazo zilifuatiliwa sana na pande mbalimbali kimataifa.
Mwitikio huo ambao ulifikia asilimia 700 ulipokea mapendekezo yenye thamani ya jumla ya dola za kimarekani bilioni 14, kiasi ambacho kilizidi lengo lililowekwa la dola bilioni 2. Pesa ambazo zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kulipa madeni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya uwekezaji inaeleza kuwa mafanikio hayo sasa yatapunguza kiwango cha ukopaji kutoka masoko ya mitaji ya ndani na kuelekeza nguvu katika masoko ya kimataifa.
No comments