Tumbatu,Upungufu wa wanafuzi wanaoenda kufanya mafunzo ya vitendo vijijini.
Idadi ya wanafunzi kutoka chuo cha kiislamu Mazizini Unguja
wanaochagua kufanya mafunzo ya vitendo
kwa shule za vijijini inaripotiwa kupungua siku hadi siku ikilinganishwa
na miaka iliyopita.
Akizungumza na Radio Tumbatu
fm katika ziara ya ukaguzi wa wanafunzi alie pangwa kusimamia shule za Tumbatu mkufuzi Ali Ali Machano
kutoka chuo cha kiislam Mazizini amesema kuna tofauti kubwa ya ushiriki wa
wanafunzi hao jambo ambalo amesema linarudisha nyuma maendeleo ya wanafuzi
kutokana na kukosa msaada wa ndugu zao.
Akitoa tadhimini ya
wanaafunzi waliofika shule za Tumbatu amesema kwa mwaka 2017 walikuwa na
wanafunzi 5 na mwaka huu ni mwanafunzi mmoja.
Kwa upande wake Bi
Mwanapili Mwinyikadhi ambae pia ni mshiriki wa ziara hiyo amesema ukaguzi ni
muhimu na unasaaidia kumjenga mwanafunzi katika kukabiliana na changamoto za
kazi.
Ziara za ukaguzi wa wanafunzi wa faani ya ualimu hufanyika
kila mwaka baada ya kukamilika muhula wao masomo .
No comments