Jamii nchini imeshauriwa kuchukua taahadhari juu ya majanga ya moto
Jamii nchini imeshauriwa kuchukua taahadhari juu ya
majanga ya moto kwa kuzifanyia nyumba zao fitingi nzuri ya umeme na kufunga
kifa cha aina ya soketi breka ili kupunguza ajali za moto zinazothiri maisha ya
watu na mali zao.
Ushauri huo umetolewa na Shaabani Seif Mohamed Mkurugenzi
mtendaji wa kamisheni ya kukabiliana na maafa zanzibar wakati alipofika kumfariji na kumpa pole
mzazi wa mtoto aliefariki kwa ajali ya
moto tariki abubakar said mkazi wa
eneo la kwa mtumwajeni wilaya ya mjini.
Amesema kuwa ufungaji wa fitingi usio fata mpangilio
mzuri unaweza kusababisha ajali.
Aidha, Mkurugenzi huyo amewaomba wananchi ambao
nyumba zao ni za zamani kuangalia uwezekano wa kuzifanyia upya fitingi kwa
kuondosha waya zilizopita ndani ya kuta za nyumba na kuzipitisha katika bomba
maalum za kupitishia waya ili iwe rahisi kuzuwia athari zitakazojitokeza.
Nae Sheha wa Shehia ya kwa Mtumwajeni Rajab Ali Ngauchwa
ameishukuru serikali kuanzia ngazi ya wilaya na uongozi wa kamisheni ya
kukabiliana na maafa kwa kufika kwao kuifariji familia ilipatwa na msiba
sambamba na kuwaomba wananchi kuwa na uwangalifu wa hali ya juu katika utumiaji
wa vifaa vya umeme kutokana na majanga ya moto kuengezeka na kusababisha vifo.
kwa upande wake mama Mzazi aliefiwa na mwanawe Bi
Khadija khamis Salum ameiomba serikali na wadau mbali mbali kumsaidia baadhi ya
vifaa ili aweze kurejesha hali kutokana na vifaa vyake vyote kutekea kwa moto
ikiwemo saruji, mabati, milango, nguo pamoja na vyombo.
No comments