Amchoma mwanafunzi kisu kisa maembe
Kutoka nchini Kenya, mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha Chuka, amechomwa kisu mmiliki wa nyumba aliyopanga baada ya kuchuma maembe ya mwenye nyumba hiyo kwenye mwembe ulio ndani ya eneo wanaloishi.
Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano February 21, 2018 na kuthibitishwa na OCPD wa eneo hilo la Meru Kusini Baraza Saiya ambapo ameeleza kuwa mwanafunzi mwingine amepata majeraha ya kisu pia kutoka kwa mwenye nyumba huyo wakati akitaka kumtetea mwenzake.
Saiya amesema kuwa mwenye nyumba huyo pia alichomwa visu na wanafunzi wa chuo hicho kama kulipa kisasi kwa alichomfanyia mwanafunzi mwenzao, na baadaye watatu hao wamepelekwa hospitali kwaajili ya matibabu.
Mwenye nyumba hiyo tayari anashikiliwa na polisi na kwamba anasubiri kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo.
No comments