TUMBATU FM

Breaking News

Liverpool yaibamiza West Ham United 4-1



Liverpool imezidi kudhamiria kuwa inauhitaji ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza baada ya kuilaza vilivyo West Ham United kwa mabao 4-1. Mtangange ukipigwa Anfield.

Katika mchezo huo, mabao ya Liverpool yametiwa kimiani na Emre Can (29'), Mohamed Salah (59'), Roberto Firmino (57') na Sadio Mane akipigilia msumari wa mwisho (77').

Bao pekee la West Ham limefungwa na Antonio (59').

Matokeo haya sasa yameipeleka Liverpool mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi, huku Manchester United ikishuka hadi nafasi ya 3
.

No comments