TUMBATU FM

Breaking News

Marekani imepanga kuhamisha ubalozi wake Jerusalem mwezi Mei



Marekani inatarajia kuuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv mpaka Jerusalem ifikapo Mei 14.

Mnamo Mei 1948 taifa la Israel lilitengenezwa na litakambuliwa na Washington tarehe kama hiyo.

Msemaji wa Marekani Heather Nauert amesema kuwa Marekani itauhamisha ubalozi wake Jerusalem katika siku ya kuadhmisha miaka 70 ya taifa la Israel.

Ubalozi wa sasa wa Marekani ulio Tel Aviv hautafungwa bali utaendelea kutumika kama tawi la ubalozi utakaofunguliwa Jerusalem.

Uamuzi wa Marekani kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel umepingwa na mataifa mengi ulimwenguni.

Licha ya hivyo Marekani imeonyesha kutojali.

No comments