TUMBATU FM

Breaking News

Somalia: Idadi ya vifo kutokana na milipuko mjini Mogadishu yaongezeka



Idadi ya vifo kutokana milipuko nchini Somalia imeongezeka kuanzia 18 mpaka kufikia 45.

Kwa mujibu wa habari,kundi la Al Qaeda lenye uhusiano na Al Shabaab ndilo liemhusika katika kutekeleza shambulizi hilo.

Shambulizi hilo lililolenga ikulu ya rais na hoteli karibu yake limesababisha watu wengine 36 kujeruhiwa.

Inasemekana kuwa watu 21 katika hoteli hiyo walipoteza maisha wakati shambulizi hilo lilipotokea.

Afisa wa polisi mjini hapo yeye amesema ana uhakika na vifo 36.

Kundi hilo linadai kuwa linataka kuiondoa serikali.

No comments