Dalali alitaka tawi la Simba Cream kuanzisha timu ya Vijana chini ya miaka 17
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Simba, Hassani Dalali amelitaka tawi la Simba Cream la Jijini Tanga kuanzisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ili iweze kuwa hazina kubwa ya wachezaji kwa siku za mbeleni.
Licha ya hivyo lakini pia inasaidia kuweza kuinua vipaji vya wachezaji wachanga ambao wanaweza kuonekana thamani yao siku zinazokuja kwani mkoa wa Tanga una vipaji vya soka vingi.
Dalali aliyesema hayo juzi akizungumza na wanachama wa Simba ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huukatika tawi la Simba Cream la Tanga mjini ambalo lilianzishwa mwaka 2013 na kuzinduliwa na aliyekuwa Rais wa Simba Evans Aveva.
Alisema uanzishwaji wa timu hiyo utakuwa na faida kubwa kwa kusaidia timu hiyo kuwa na hazina ya wachezaji ambao wanaweza kuwatumia kwa miaka ijayo ili kuendelea kuwika kama ilivyokuwa miaka ya nyuma hapa nchini.
“Kwani timu hiyo inapoanzishwa na kuweza kuwa imara itatuwezesha tunapotaka wachezaji tunakuja kuchukua mkoani Tanga kwa sababu tutakuwa tumewekeza mtaji mkubwa wa vijana”Alisema.
Hata hivyo alisema tawi la Simba la Kinondoni kwa miaka ya nyuma ndio ambalo liliwasaidia kuwapelekea mchezaji Uhuru Selemani na baadae yeye kumpeleka kwenye klabu ya Coastal Unon .
No comments