TUMBATU FM

Breaking News

Vurugu za Mashabiki zasababisha Polisi mmoja Kuuaw



Afisa Polisi mmoja amefariki hapo jana kufuatia vurugu zilizofanywa na baadhi ya mashabiki wa klabu ya Spartak Moscow dhid ya wale wa timu ya Athletic Bilbao kabla ya mchezo wa Europa League hapo jana siku ya Alhamisi.

Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuwasha baruti zilizokuwa zikiwaka katika mitaa zilizosababisha baadhi ya mashabiki wa Bilbao kufikishwa hospitali.

Kufuatia machafuko hayo askari polisi mmoja alifariki kutokana na shinikizo la moyo.

Msemaji wa jeshi la polisi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho huku akishindwa kueleza chanzo cha umauti wake.


Askari huyo alifariki baada ya kufikishwa hospitalini kwaajili ya matibabu8 kufuatia kupata shinikizo la moyo wakati akijaribu kutuliza vurugu za mashabiki eneo la Basque.


Shirikisho la soka barani Ulay (UEFA) limesema kuwa limesikitishwa na  tukio hilo lililojitokeza huko Bilbao usiku wa siku ya Alhamisi.

No comments