TUMBATU FM

Breaking News

Hatua iliyo fika SMZ tatizo la usafiri Pemba kwenda Tanga

pemba
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inaendelea na jitihada za kulipatia Ufumbuzi tatizo la ukosefu wa Usafiri wa Uhakiki wa kutoka pemba kwenda Tanga ili wananchi waweze kunufaika na huduma ya usafiri.
Naibu waziri wa Wizara ya ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Muhammed Ahmada amesema serikali inatambua tatizo la ukosefu wa Usafiri na tayari inazungumza na kampuni ya Azam Marine kuharikisha matengenezo ya Meli ya Sea link2 ili iweze kutumika kwa usafiri wa Pemba kwenda Tanga.
Amesema kuwepo kwa tatizo la Ukosefu wa Usafiri Visiwani humo kunatokana na kuharibika kwa meli hiyo ambayo imepata hitilafu ya Engine na kusababisha kukatisha huduma za usafiri kwa abiria hao.
    Aidha Naibu Ahmada ametowa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kupanda majahazi ili kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa safari hususani katika kipindi cha Upepo ili kuweza kupunguza Upotevu wa mali za abiria pamoja na vifo.

No comments