TUMBATU FM

Breaking News

Wavuvi Ishrini wanusurika kufa baharini

Image result for Images wavuvi

Mkurugenzi  mtendaji Ndg  Shaabani Seif Mohamed wa kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar amewataka  wamiliki na manahodha wa vyombo vya  baharini kuwa na mawasiliano ya uhakika kwa lengo la kutoa taarifa pindi hitilafu zinapotokea wanapokuwa baharini.

Kauli  hiyo ameisema katika kituo maalum cha uokozi cha kmkm kibweni wakati akiwapokea  wavuvi ishirini na tatu waliokolewa wakiwa hai  katika eneo la mkwaja na kipumbwi tukio lilosababishwa na hitilafu iliosababisha chombo chao kukata moto wakiwa safarini kuelekea mavuvini mwao.

Aidha, amelezea kusikitishwa kwake na nahodha wa chombo kimoja kilichokataa kutoa msaada kwa chombo cha snepa namba mbili kwa madai ya kwamba waachwe wakavue  na baadae ndipo waje kuwakoa kitendo ambacho sio kizuri ukizingatia ajali za baharini kila mmoja  inaweza ikamkumba.

Akielezea  kutokea kwa tukio hilo nahodha wa chombo cha snepa namba mbili  Issa Khamis Dadi amesema chombo chao kimepotea siku ya jumamosi baada ya kupata hitilafu na kuzimika hafla kwa mashine yao majira ya saa saba usiku na kupelekea kukaa baharini kwa muda wa siku nne.

Sambamba  na hayo nahodha Issa ameleza kuwa jitihada za zoezi la kuwatafuta lilikua gumu kutokana na bahari kuchafuka kulikosababishwa na upepo mkali lakin, huku wakitoa shukuran kwa kikosi maalum cha kuzuia magendo (kmkm) kwa kufanikisha zoezi la uokozi.

Wavuvi  wote ishirini na tatu wamepokelewa wakiwa salama na kuwahishwa katika hospitali kuu ya mnazi mmoja kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi. 

No comments