Rais aeleza kuwepo matumiz mabya kwenye shirika la nyumba za Taifa NHC
Rais DK. John Magufuli, ameeleza kuwapo kwa matumizi mabaya ya fedha ndani ya shirika la nyumba la Taifa (NHC) na kwenye taasisi za fedha kwa kuhusisha viongozi na wafanyakazi.
Hujuma hizo zilifichuliwa jana kwa nyakati tofauti na Rais Magufuli wakati wa uziduzi wa nyumba 150 zilizojengwa na NHC katika eneo la Iyumbu na uzinduzi wa tawi la benki ya CRDB mkoani Dodoma.
Rais Magufuli alisema licha ya kazi nzuri inayofanywa na NHC, lakini bado kunadosari, hasa katika matumizi ya fedha.
“Mnafanya kazi nzuri, lakini matumizi yenu si mazuri, yako mengi ninayoyajua na tuhuma zipo.
“NHC mmeshakopa sh bilioni 360, iko miradi inayoendelea vinzuri, lakini kunawakati matumizi ya fedha hayakuwa mazuri. Ndio maana tulizua suala la kukopakopa kwa sababu baadaye mzigo huu utakuja kubebwa na serikali.
“Serikali haitoi ‘guarantee’ mahali ambako bado kuna mashaka fedha yake inatumikaje.
“Asanteni sana kwa kulia mbele ya watanzania na mimi nataka kuwaeleza kilio chenu sasa kiwafundishe namna ya kutumia vinzuri fedha za serikali, ni lazima mtu ajuifunze kumeza kile kinachopita kwenye koo,” alisema Rais Magufuli.
Alilitaka shirika hilo kujitathimini kwa kuondoa doasari ndogondogo alizonazo ili kwenda katika mlengo anaoutaka.
“Jengeni nyumba kila mahali, lakini angalieni matumizi yenu, nataka NHC itemize wajibu wake kwa manufaa ya watanzania… mengine yote ni safi, tatizo ni matumizi yafedha na maujanja ujanja Fulani,” alisema.
No comments