Serikali ya mapinduzi Zanzibar ya laani kuwawa kwa Asikari Nchin Congo
Serikali ya mapuindizi ya zanziba imelaani kuuwawa kwa
majeshi ya ulinzi ya Tanzania nchini congo na kuziomba familia zilizopoteza
ndugu zao kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki kwa kuwa wote ni njia moja .
Wanajeshi hao walikuwa nchini kongo wakifanya kazi ya kulinda
amani, tukio lililotokea disemba 7 mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kupokea miili hiyo kwenye
kambi ya jeshi migombani mjini zanziba , makamo wa pili wa Rais balozi seif ali
idd amesema kuwa tukio lililotokea ni la kusikitisha kutokana na
wanajeshi hao kuuwawa wakiwa kazini na kuziomba familia kuendela kuwa
watulivu kwa kuwa serikali ipo nao bega kwa bega katika
shughuli hiyo.
Waziri wa nchi ofisi ya rais, idara maalum na vikosi
vya smz haji kheri amesema wameshtushwa na shmbulio lililowapata
wanajeshi hao na kusema kuwa kamwe hawatokata tamaa kupeleka wanajeshi katika
nchi mbalimbali kusimamia amani.
Wanajeshi hao walioipoteza maisha nchini kongo
wakitokea zanziba ni pamoja na nassor daud ,ali haji ussi , iddi abdalla ali
,juma mossi ali , mwinchum, issa mussa juma , hassan abdallah makame na hamad
mzee kamna ambao wametokea kisiwani unguja huku hamad
haji bakar akitpokea kisiwani pemba.
No comments