Muume na Mke wakatwa kwa panga Singida
Mume na mke wakazi wa kitongoji cha Kidogue wilayani
Mkalama wamefariki dunia kwa madai ya kukatwa mapanga shingoni na kichwani na
watu wasiojulikana.
Mauaji ya wanandoa hao, Kija Kitundu (53) na mkewe Mwajuma Ramadhan (59) yalitokea Desemba 10 saa sita usiku nyumbani kwao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba alisema watoto wa wanandoa hao, Ramadhani (14) na Namagalu (12), wamepelekwa hospitali kwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo.
Magiligimba alisema siku ya tukio wauaji hao walitumia ngazi kupanda juu ya paa la nyumba ya Kija kisha kuingia chumbani kwa wanandoa hao na kuwacharanga mapanga.
Alifafanua kuwa kabla ya tukio hilo, kuna mtu alikwenda nyumbani kwa Kija kuomba pampu lakini aliponyimwa ndipo ugomvi ukaanza baina yao.
Chazo - Mwananchi
No comments