WANAFUNZI 19,242 WACHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018 SIMIYU
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini akifungua kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani humo, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Afisa Elimu Mkoa, Mwl. Julius Nestory akiwasilisha taarifa ya hali ya ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kwa mwaka 2017, katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wiayaya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akichangia hoja katika katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwiburi akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Wilaya ya Meatu, Veronica Kinyemi akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndg.Anderson Njiginya, akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa, Mhandisi Paul Jidayi akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Itilima, Mahamoud Mabula akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoaani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Mji wa Bariadi, Ndg.Melkezedeck Humbe akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, Mkoani Simiyu kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
****
Jumla ya wanafunzi 19,242 mkoani Simiyu sawa na asilimia 92.5 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari katika awamu ya kwanza kwa mwaka 2018.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Ndg.Jumanne Sagini katika kikao cha kutangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2018 kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Sagini amesema jumla ya wanafunzi 20,818 sawa na asilimia 67.73 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba walifaulu, ambapo kati yao 1576 sawa na asilimia 7.5 ya waliofaulu hawakupata nafasi ya kuanza kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika baadhi ya Halmashauri.
“Wanafunzi waliokosa nafasi Halmashauri ya Mji wa Bariadi ni wale waliopaswa kwenda Shule ya Sekondari Kidinda(207) na Biashara(162), Halmashauri ya Wilaya ya Busega walipaswa kwenda shule za Lamadi (486), Nasa (358) na Sogesca (363). Ni wajibu wa Halmashauri hizi kushirikiana na wananchi kuhakikisha miundombinu pungufu imekamilishwa haraka ili ifikapo Februari 15, 2018 wanafunzi hao waripoti kwenye shule walizopaswa kwenda” ,amefafanua Sagini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Halmashauri ya Mji Bariadi wamesema, Halmashauri zao zinaendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hizo na wataendelea kufanya jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha kuwa miundombinu hiyo pungufu inakamilika haraka, ili kufikia Februari 05 mwakani wanafunzi wote waliokosa nafasi awamu ya kwanza waweze kwenda shule.
Wakati huo huo Sagini amezitaka Halmashauri kuendelea kushirikiana na wadau wote wa elimu kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2018 bila vikwazo vya aina yoyote.
Ameongeza kuwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla washirikiane na uongozi wa wilaya, halmashauri na shule kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliochaguliwa wanaandikishwa, wanaripoti shuleni na kuendelea na masomo yao kwa bidii hadi watakapomaliza elimu yao ya sekondari mwaka 2021.
Akielezea hali ya ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa mwaka 2017, Afisa Elimu Mkoa, Mwl. Julius Nestory amesema kwa mara ya kwanza mwanafunzi aliyeongoza katika Mkoa ambaye ni (msichana) Hoka Lyaganda Saguda ametoka katika Shule ya Serikali ambayo ni Shule ya Msingi Sima B iliyopo Mjini Bariadi.
Amesema ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu na kuinua kiwango cha ufaulu mkoani humo Mikakati ya kuinua ufaulu ya kila wilaya isimamiwe kikamilifu, Ofisi za Wilaya, Halmashauri, Kata na Wakuu wa Shule zifanye ufuatiliaji kuhusu ufundishaji na ujifunzaji na Ukaguzi wa shule ufanyike kwa kiwango kisichopungua asilimia 50 kwa mwaka na Wakurugenzi watenge fedha kwa ajili ya ukaguzi wa shule.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Itilima, Mhe.Mahamoud Mabula ameshauri kuwa ili kuinua ufaulu suala la maendeleo ya Elimu liwe agenda ya kudumu katika vikao vyote muhimu vya Halmashauri mkoani humo, ili kutoa nafasi ya kujadili changamoto mbalimbali za sekta ya elimu na kuzitafutia ufumbuzi.
Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu imeongezeka kutoka wanafunzi 16,620 mwaka 2017 hadi wanafunzi 19,242.
Imeandaliwa na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.
No comments