Picha : RAIS MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA TISA WA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA (UWT) MJINI DODOMA
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM , Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa mkutano Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kabla ya kufungua mkutano wao wa Tisa uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Wajumbe wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakishangilia kabla ya ufunguzi wa mkutano huo wa tisa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akivalishwa Kitambaa kichwani mara baada ya kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkutano wa tisa wa (UWT) uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kuhamia rasmi katika Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiimba nyimbo za CCM pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wa pili kutoka (kushoto), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wa pili kutoka (kulia), Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakwanza kulia mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akishangilia katika mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo mara baada ya kufungua mkutano huo wa tisa wa (UWT) mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Mama Maria Nyerere ambaye pia alihudhuria katika mkutano huo wa wa Tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza katika mkutano huo wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa CCM, Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na bendi ya Tanzania One Theater TOT wakati ikitumbuiza katika mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akicheza pamoja na wajumbe wengine wa UWT mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza jambo na Mama Maria Nyerere mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT uliofanyika mjini Dodoma. PICHA NA IKULU
No comments