MAHARAMIA WA KAZI ZA WASANII KUFIKISHWA MAHAKAMANI WIKI IJAYO
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Mzigo ambao mpaka sasa umeshakamatwa ukiwa umeifadhiwa.
***
Picha/Habari na Kajunason/MMG-Dar es Salaam.
Maharamia wa kazi za wasanii zaidi ya 200 waliokamatwa katika zoezi laukamataji kazi feki za sanaa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa kwa sasa anaishukuru serikali kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonyesha kwa kuwa bega kwa bega kwa vile wamekuwa wakinyonya wasanii.
"Ndugu zangu waandishi nimewaita hapa kuwaeleza juu ya zoezi la kumkamata maharamia wa kazi za sanaa bado linaendelea vizuri na sasa wanatarajia kufikishwa mahakamani wiki ijayo ili waweze kusomewa mashtaka yao," alisema Msama.
Msama alisema kuwa mpaka sasa msako huo umefanikisha kukamata vifaa vya zaidi ya bilioni 1 ambavyo ikiwemo kopyuta, laptop na cd feki.
Aliongeza kuwa watanzania lazima walipe kodi na wauze kazi zilizo na stika za mapato (TRA) ili wasanii wapate mapato na serikali ipate mapato.
"Wamachinga acheni kulalamika, mnaopoenda kununua Filamu za nje na ndani hakikisheni Filamu hiyo ina Stika ya TRA, ukiuza yenye Stika mtu hatokukamata", amesema Msama.
Msama aliwaomba Watanzania watambue awamu hii ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli haitaki ujanja ujanja, lazima kufanya kazi kwa bidii ili upate kipato halali.
Hata hivyo, zoezi laukamataji Kazi feki za sanaa litaendelea katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni zoezi la nchi nzima.
No comments