Wakulima wazungu nchini Zimbabwe, warudishiwa mashamba yao.
Serikali ya mpya ya Zimbabwe chini ya Rais
Emmerson Mnangagwa, kupitia kwa Waziri wake wa Kilimo Perence Shiri imetoa amri kurudishwa mashamba
yaliyokuwa yakimilikiwa na wakulima Wazungu, ambao walinyang’anywa wakati wa
utawala wa Robert Mugabe na kupewa raia wa Zimbabwe.
Waziri Shiri amesema kuwa wale ambao wana
vibali rasmi wataruhusiwa kuendelea kulima katika mashamba hayo ili kuhakikisha
uzalishaji. Shiri amesema hatua hiyo inalenga kukuza kilimo kwa ajili ya uchumi
wa nchi hiyo ambao unaendelea kudorora kila kukicha.
“Ikiwa tunataka kufanikisha malengo yaliyowekwa na
serikali ni lazima tutumie kilimo kama nguzo ya uchumi, lazima tuhakikishe
utaratibu mzuri wa kilimo,” – Perence Shiri
No comments