Rais Maguful aahidi kulipa madeni ya Walimu
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kulipa
madeni ya walimu takribani shilingi Bil. 25 mara baada ya viongozi wa Chama cha
Walimu Tanzania (CWT) kuthibitisha uhalali wa madeni hayo.
Rais Dkt. Magufuli ametoa tamko hilo jana Mjini Dodoma
,alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa CWT ambao umehusisha wawakilishi kutoka
Mikoa yote ya Tanzania Bara . “Ninawaahidi walimu wenzangu, mara baada ya zoezi
la uhakiki kuisha wale walim ambao wanadai malipo halali watalipwa,”alifafanua
Rais Dkt. Magufuli.
Aliendelea kusema kuwa kabla hajawa Rais alikuwa mwalimu hivyo
anazifahamu vizuri shida za walimu hivyo walimu wajisikie wana muwakilishi
mzuri.
Aidha, Rais Magufuli amewataka viongozi wa CWT
wa wilaya na mikoa kuhakiki madeni ya walimu ya maeneo yao na kuyawasilisha kwa
Waziri Mkuu kwa ajili ya kulipwa.
Rais Dkt. Magufuli amesema Serikali ya awamu
ya Tano imeendelea kufanya jitihada za kuboresha maslahi ya walimu ambapo tangu
imeingia madarakani jumla ya shilingi bilioni 56.92 zimetolewa kwa ajili ya
kulipa madeni ya walimu ambapo kati ya fedha hizop, shilingi bilioni 14.23 ni
madeni ya mishahara na shilingi bilioni 42.69 ni madeni yasiyo ya mishahara.
Vile vile Rais Magufuli amewasihi walimu
wenzake kupokea kile kidogo ambacho Serikali inakitoa wakati huu ambapo
Serikali inawekeza katika kutekeleza miradi mbalimbali kama vile miradi ya
afya, umeme, maji, barabara na reli. Miradi ambayo inawagusa pia walimu katika
maisha yao ya kila siku nawanapotimiza majukumu yao.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amewaahidi
walimu hao kufanyia kazi maombi mbalimbali ambayo wamewasilisha ikiwemo
kurudisha posho ya kufundishia pamoja na Serikali kutoa mikopo isiyo na riba
ili kuwasaidia kujenga nyumba za kuishi.
Hata hivyo, amewata viongozi husika
kushughulikia uwiano sahihi wa walimu wa shule za msingi na sekondari walioko
mijini na vijijini kutokana na walimu wengi kupangiwa mijini.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais CWT Leah Ulaya
alisema kuwa wanaimani na Rais Magufuli na juhudi zake zinaonekana wazi katika
kupambana na ufisadi, uzembe, rushwa, uhujumu uchumi na vita dhidi ya madawa ya
kulevya.
No comments