TUMBATU FM

Breaking News

Umoja wa Afrika umetoa taarifa ukilaani uamuzi wa rais Donald Trump


Umoja wa Afrika umetoa taarifa ukilaani uamuzi wa rais Donald Trump wa Marekani kuhusu suala la Jerusalem.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imesema, uamuzi wa rais wa Marekani utazidisha hali ya wasiwasi ya kikanda, pia utaleta athari mbaya kwa utatuzi wa amani wa suala la Palestina na Israel.

Umoja wa Afrika umesisitiza kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wananchi wa Palestina katika kujenga nchi yao huru ambayo Jerusalem Mashariki ni mji mkuu wake.

Jumatano wiki hii, Rais Trump alitangaza kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, vilevile Marekani itaanza mchakato wa kuhamisha ubalozi wa Marekani nchini Israel kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem.

No comments