TUMBATU FM

Breaking News

Jeshi la polisi zanzibar limesema limejipanga upya udhalilishaji






Jeshi  la polisi zanzibar limesema limejipanga upya katika kuhakikisha vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia vinaondoka kabisa katika visiwa vya zanzibar kwa kuwachukulia hatua wale wote wanaofanya matendo hayo , ambayo ni kinyume na sheria .

Hayo  yamejiri mara baada ya  jeshi la polisi mkoa wa mjini maghrib  kupitia dawati la jinsia  kutimiza siku kumi na sita za kupinga vitendo vya  udhalilishaji kwa kutoa elimu kwa wananchi ni   namna  gani ya kujikinga  dhidi  ya vitendo hivyo 

Akizungumza  katika kilele cha siku 16 za kupinga udhalilishaji kwa dawati la polis mkoa wa mjini , naibu waziri wa kazi, uwezeshaji, vijana wazee wanwake na watoto shadya  mohamed suleiman amesema  jeshi hilolina jukumu la kuhakikisha hatua zinzchukuliwa ili kupunguza matendo hayo.

Aidha  shadya  amewataka  wazazi kutowaficha wahalifu wanao fanya vitendo hivyo na pindi watakapobainika, kwani hatua hiyo inawapa mwanya wafanyaji kuendelea kufanya hayo kutokana na muhali iliokithiri kwa wazazi haswa ikibainika mfanyaji wa matendo hayo ni mtu wa karibu.

Naye  nae kaimu kamishna  wa polisi  zanzibar  dcp  juma yussuf ali  amewataka wananchi kuifanyia kazi elimu waliyo patiwa sambamba na kuwaasa wazazi kujiepusha  kutumia majina yasiyofaa kwa watoto wao.


Sherehe  hizo za kuhitimisha siku 16 za kupinga udhalilishaji zimefanyika katika viwanja vya ziwani zilizokwenda sambamba na kauli mbiu ya dawati la jinsia  kwa mkoa wa mjini   ikisema funguka,acha manunguniko , lete malalamiko kituoni ili yafanyiwe kazi.

No comments