Rais Muhamadu Buhari akata utepe kukamilika mradi
Rais Muhamadu Buhari wa Nigeria amekata utepe kuashiria
kukamilika kwa mradi wa barabara iliyojengwa na Kampuni ya Uhandisi wa Ujenzi
ya China CCECC mjini Kano, kaskazini mwa nchi hiyo.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 2.1 inaunganisha barabara
kuu mbili zinazoelekea nje ya mji huo, na mradi huu umekamilika kwa miezi
minane kabla ya muda uliopangwa.
Gavana wa jimbo la Kano Abdullahi Umar Ganduje ameishukuru
kampuni ya China kwa kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha juu, na ubora wa
ujenzi pia unasifiwa sana na wakazi wa huko.
No comments