Serikali ya mapinduzi zanzibar kuandaa sheria itakayosimamia Sanaa
Serikali ya mapinduzi ya zanzibar inatarajia kuandaa
sheria itakayosimamia vyema kazi za wasanii wa zanzibar na kuhakikisha
wananufaika na kazi zao na yeyote atakayekiuka sharia kwa kutumia
kazi za wasanii kinyume na sharia atachukuliwa hatua.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa nchi ofisi
ya rais , sheria , katiba na utawala bora haroun ali suleiman wakati
akifungua mafunzo kwa wasanii kuhusiana na kazi wanazozifanya na
jinsi gani watasimamia haki zao.
Amesema kuwa serikali inatambua mchango
mkubwa unaofanywa na wasanii hapa nchini na kua inathamini kazi za wasanii hao
na ndio mana imeandaa sheria hiyo yenye lengo la kulinda na kutetea kazi
zinazofanywa na wasanii hao.
Kwa upande wake angela ndambuki ambae ni
afisa mtendaji wa kituo cha hakimiliki nchini kenya amesema kuwa lengo la
semina hiyo ni kutoa elimu kwa wasanii wa zanzibar kuhusu hakimiliki ya kazi
hizo katika mitandao pamoja ma kupata uzoefu katika kazi zao
Nae bi mtumwa khatib ameir ambae ni afisa mtendaji
wa kituo cha haki miliki zanzibar amesema baada ya semina hiyo wasanii pamoja
na watunzi watapata uelewa kuhusu matumizi ya kuweka kazi zao katika
mitandao kwa lengo la kufaidika zaidi.
Semina hiyo imeandaliwa na kituo cha haki miliki
zanzibar kwa kushirikiana na vituo vyengine vya haki miliki kenya na
malawi ili kuwapa uelewa wasanii na watunzi wengine kuhusiana
na kazi zao.
No comments