Baraza la kiswahili limewataka wazanzibar kuhakikisha wanazichangamkia fursa
Baraza la kiswahili zanzibar
(bakiza) limewataka wazanzibar kuhakikisha
wanazichangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza
haswa matumizi ya lugha ya kiswahili kwa ajili
ya kuipa hadhi lugha ya kiswahili katika
nyanja mbalimbali nchini.
Rai hiyo imetolewa mara baada ya
baraz a hilo kuandaa kongamano maalum la
kiswahili litkalofanyika desemba 19 na 20 kwa
kujumuisha wadau wa masuala ya
kiswahili kutoka nchi mbalimbali ili
kuongezea uelewa wa matumizi ya lugha fasaha ya kiswahili.
Akizungumza na waandishi wa
habari mwenyekiti wa baraza la kiswahili
zanzibar mohammed seif khatib amesema kuwa
ni vyema kwa kila mzanzibar kuipa
hadhi lugha ya kiswahili fasaha kizanzibar
huku akifahamisha lengo kuu la uandaaji
wa kongamano hilo na baraza la kiswahili hapo zanzibar
kwa upande wake katibu mtendaji
wa baraza la kiswahili zanzibar mwanahija
ali amewaomba wataalamu wa lugha ya kiswahili watumie fursa ya kongamano
hilo kuzungumza lugha fasaha ya kiswahili kutokana na nchi mbalimbal
zitashiriki kwenye kongamano hilo.
Nae Dk amour
salum mratibu wa baraza la kiswahili
zanzizbar amesema kuwa ni vyema kila mtanzania
kuhakikisha anaikuza lugha ya kiswahili popote pale kwa kuwa ni lugha
inayozungumzwa nchi mbalimbali na si afrika peke.
Kongamano la kimataifa la
kiswahili hilo ni kongamano la kwanza
kufanyika visiwani zanzibar likitarajiwa
kuendeshwa kwa takriban siku mbili ambapo
raisi wa znaizbar na mweyekiti wa
baraza la mapinduzi dk ali mohammed
shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi huo.
No comments