Adhabu kali hudumaza wanafunzi
serikali imetakiwa kuendelea
kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ili
visiathiri malezi hayo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa dodoma,
yaliyofanyika katika kijiji cha mlowa barabarani, mwanafunzi eunice mwaipopo
alisema watoto wamekuwa wakikabiliwa na ukatili ambao wakati mwingine umekuwa
ukiathiri maendeleo yao shuleni.
Alisema jamii ina wajibu wa kuhakikisha watoto
wanalindwa na haki zao zinaheshimiwa. mkazi mwingine wa kijiji hicho, yohana
magomba alitaka hatua stahiki ziwe zinachukuliwa kwa wote wanaofanya vitendo
vya ukatili dhidi ya watoto.
Alisema vitendo vya rushwa vimekuwa vikisababisha
matukio mengi ya ukatili kuishia juu juu licha ya taarifa kutolewa na wahusika
kukamatwa lakini hakuna adhabu yoyote wanayopewa.
No comments