Mrundikano wa kesi za udhalilishaji mahakamani
Jumuiya ya vijana na elimu
ya mkoa wa kaskazini unguja (juvieka) imesema bado idadi ya kesi za
udhalilishaji ambazo hazijapatiwa hukumu inaongezeka huku wananchi wakiendelea
kufuatilia mahakamani.
Akizungumza katika kilele
cha kuadhimisha siku kumi na sita za kupinga vitendo vya ushalilishaji katibu wa
jumuiya hiyo bibi hadija amesema pamoja na
kuongezeka kwa kasi ya kuripoti matukio ya vitendo vivyo bado wananchi
walio wengi wanahamu ya kusikia humu wakiamini ndio njia pekee ya kuondosha
kabisa vitendo hivyo.
Amesema kwa mwaka huu kesi
zilizopatiwa hukumu ni kidogo ikilinganishwa na idadi ya kesi zilizoripotiwa.
Aidha akifafanua zaidi
amezitaja baadhi ya kesi na kusema kwamba kuongezeka kwa kesi hizo kunawatia hofu wazazi katika malezi
ya watoto wao.
No comments