TUMBATU FM

Breaking News

Mr. Nice aapa kula sahani moja na Young Dee



Msanii wa muziki Bongo, Mr. Nice amesema atamchukulia hatua za kisheria Young Dee baada ya kutumia vionjo vya ngoma yake.
Young Dee katika ngoma yake mpya ‘Kibeni 10’ amechukua vionjo kutoka kwenye ngoma ya Mr. Nice ‘King’asti’. Akizungumza na The Playlist, Times Fm Mr. Nice amesema hamfahamu Young Dee na alichokifanya ni kinyume na sheria.
“Sijamruhusu yeyote kufanya remix ya ngoma zangu kwa hiyo ni mtu amejiamulia mwenyewe na hajawahi kuwasiliana na mimi, kwanza simjui na ningekuwa namjua angalau ningesema, simjui Young Dee ni nani nafanya kumsikia tu kama ninavyosikia wengine” amesema.
“Ninachokifanya ni kuwasilisha sehemu husika waseme naye kwa sababu najua wao ndio wenye jibu lake na ili iwe fundisho na kwa wengine wenye tabia kama hizo” ameongeza.
Mr. Nice si msanii wa kwanza kwa mwaka huu kutoa kauli kama hiyo, utakumbuka TID alitishia kuwafikisha mahakamani kundi la OMG pamoja na Quick Rocka baada ya kuchukua vionjo vya ngoma yake ‘Watasema Sana’ katika ngoma yao lakini baadaye suala  hilo likaisha bila kufika huko.

No comments