Young Dee adai amefanya ‘Kiben 10’ kutambua mchango wa Mr Nice
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Young Dee amefunguka kwa kudai kuwa amefanya wimbo ‘Kiben 10’ kupitia style ya TAKEU ya Mr Nice ili kuonyesha kwamba muimbaji huyo wa zamani alifanya kazi kubwa sana kwenye muziki mpaka sasa wasanii wanalipwa pesa nyingi katika show zao.
Rapa huyo ameiambia Bongo5 kuwa hakuzungumza chochote na mkongwe huyo mpaka inatoka project hiyo ili kumfanyia surprise.
“Ngoma ndani yake kuna wasanii wengi sio mimi peke yangu kama unavyousikiliza, ni ngoma fulani ya kukubali kile kikubwa ambayo kimefanya na wasani wakongwe waliopita kwenye game,” alisema Young Dee.
Aliongeza, “Unapomzungumzia Mr Nice ni jina kubwa sana kwenye muziki wetu, ni msanii ambaye amefungua njia kwa wasanii wengi, ngoma zake pamoa na style yake ya Takeu ilifanya vizuri kila kona mpaka nje ya mipaka hata leo hizo shows watu wanalipwa mamilioni alianzisha yeye hiyo system,”
Rapa huyo amesema bado hajajua kama ataachia video ya ngoma hiyo huku akiwataka mashabiki wa muziki kuisikiliza ili kupata vitu hadimu ambavyo amedai vinapatikana katika ngoma hiyo.
No comments