Rais wa zanzibar afanya uteuzi mpya
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi amefanya Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena A. Said imesema kuwa walioteuliwa ni
1. Ndugu Mussa Haji Ali ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu.
2. Ndugu Habiba Hassan Omar ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.
3. Ndugu Issa Mahfoudh Haji, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.
4. Ndugu Aboud Hasssan Mwinyi, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Anaeshughulikia (Fedha na Mipango).
5. Ndugu Mikidadi Mbarouk Mzee, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.
Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 10 Julai, 2021.
Aidha wateuliwa wote waliotajwa wataapishwa siku ya Jumatatu tarehe 12 Julai, 2021 saa 4.00 asubuhi – Ikulu Zanzibar.
Wakati huo huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi ametengua Uteuzi wa Wakurugenzi kuanzia leo tarehe 10 Julai, 2021.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena A. Said imesema kuwa waliotenguliwa ni kama ifuatavyo:
Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto:
1) Dkt Fadhil Mohammed Abdulla Mkugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya.
2) Ndugu Ramadhan Khamis Juma, Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji.
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na idara Maalum za SMZ:
1) Ndugu Ali Abdalla Said Natepe, Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Magharibi “B”.
2) Ndugu Makame Mwadini Silima, Mkurugenzi wa Baraza la Mji Kaskazini “B”
3) Ndugu Muhamed Salum Muhamed, Mkurugenzi Baraza la Mji Kati.
4) Ndugu Kassim Mtoro Abu, Mkurugenzi wa Halmashauri Kusini, Unguja.
Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda:
1) Ndugu Abdulhamid Idrissa Haji, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati (SMIDA).
No comments