Rais Samia atuma salamu za pole na kutoa agizo kwa vyombo vya usalama
Rais Samia atuma salamu za pole na kutoa agizo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla na wafanyabiashara wa kariakoo kwa kuunguliwa na soko hilo hapo Jana Julai 10,2021.
Aidha Rais Samia ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo cha moto huo.
Wakati huo huo Rais Samia pia ametuma salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martin Shigella na Jumuiya ya Kiislamu Tanzania kufuatia kuungua moto kwa Bweni la shule ya sekondari ya wasichana ya Kiislamu AT-TAAUN.
No comments