TADIO imeendesha mafuzo ya maadidi kwa mameneja wa radio za kijamii
Shirika la habari za maedeleo Tanzania TADIO ambalo ni mwavuli wa radio za kijamii nchini Tanzania limeendesha mafuzo ya maadidi ya wandishi wa habari ili kuwajengewa uwezo wa kufanyaazi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Katka mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo mameneja wa vyo mbo vya habari mratibu wa shirika la TADIO Cosmas Lupoja amewakumbusha majukumu yao na kuwasisitiza kuwa na utaratibu wa kupatanisha jamii badala ya kuripoti mizozo inayotokea siku hadi siku.
Amesema ni muhimu katika vipindi vya uchaguzi waandishi wanatakiwa kukumbushwa masuala ya maadili ya habari ili kuepuka mkanganyiko na kutumbukia kwenye migogoro baina yao na na jamii au na serikali.
Akichangia maada ya utambuzi ya migogoro katika mafuzo hayo meneja wa Dodoma FM Zania Miraji amesema mafuzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo shirika la TADIO kwa kushirikiana na UNESCO wanawajengea uwezo wa hali ya juu wasimamizi wakuu wa vyombo hivyo vya habari ili kudhibiti mizozo na visa vya uvunjifu wa sheria na kanuni za uandishi wa habari kwa wafanyakaziMafuzo hayo ya siku sita yanajumuisha Jumla ya viongozi 35 wa vyombo vya habari vya kijamii nchini Tanzania yanafanyika huko Morogoro katika hotel ya Kingsway eneo la Msamvu.
Na Juma Haji - Tumbatu FM
No comments