Yanga yaaga Ligi ya Mabingwa Afrika
Yanga imeondolewa rasmi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia suluhu ya 0-0 dhidi ya Township Rollers jioni hii.
Township Rollers wamefanikiwa kusonga mbele mpaka hatua ya makundi, baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam, kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kazi nzuri waliyoifanya Township kwenye mechi ya awali, inawafanya Yanga kuyaaga rasmi mashindano hayo na kuwafanya waangukie Kombe la Shirikisho Afrika ambalo Simba anashiriki.
Baadaye Simba SC nayo itakuwa ina kibarua kuanzia majira ya saa 2 na nusu usiku, kukipiga dhidi ya Al Masry huko mjini Port Said, Misri.
No comments