TUMBATU FM

Breaking News

Spurs yatua hatua ya nusu fainali michuano ya FA Cup



Klabu ya Tottenham imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya FA Cup kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991 baada ya kuifunga Swansea kwa jumla ya mabao 3 – 0 mchezo uliyopigwa dimba la the Liberty hii leo siku ya Jumamosi.
Licha ya kukosekana kwa mshambuliaji hatari wa timu hiyo Harry Kane kufuatia majeraha yanayomkabili lakini wachezaji, Christian Eriksen na Erik Lamela waliweza kuisaidia timu hiyo kuchomoza na ushindi huo mnono.
Meneja wa Spurs, Mauricio Pochettino anatazamiwa kutwaa kikombe hicho kwa mara yake ya kwanza ndani ya kikosi hicho.
Kikosi cha Swansea: Nordfeldt (7), Naughton (5), Van der Hoor (6), Bartley (5), Mawson (6), Olsson (6), Ki (5), Carroll (5), Clucas (5), Dyer (5), Abraham (5).
Wachezaji waakiba: Roberts (n/a), Routledge (n/a), Narsingh (6).
Kikosi cha Tottenham: Vorm (7), Trippier (7), Sanchez (7), Vertonghen (7), Davies (7), Dier (7), Sissoko (7), Lamela (8), Eriksen (9), Lucas Moura (7), Son (8).
Wachezaji waakiba: Alli (n/a), Llorente (6).
Mchezaji bora wa mechi hiyo ni Christian Eriksen.

No comments