waandishi wa habari wametakiwa kutoa elimu kupitia vyombo vya habari juu ya athari za mvua
waandishi wa habari wametakiwa kuendelea kutoa elimu
katika vyombo vya habari juu ya athari za mvua za masika ili wananchi waweze
kujikinga na athari za mvua hizo ambazo zinasababisha hasara kubwa kwajamii.
akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari
ofini kwake maruhubi juu ya muelekeo wa mvua hizo mkurugenzi mtendaji wa
kamisheni ya kukabiliana na maafa zanzibar shaabani seif amesema vyombo vya
habari ni sehemu kubwa inayoaminika katika jamii hivyo watakapo endelea kutoa
elimu itaweza kupunguza athari za mvua kwa wananchi.
amesema
kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa mvua za masika zinatarajiwa kunyesha kwa
wastani mkubwa hivyo ni vyema kwa vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa
wananchi juu ya kujikinga na maafa yanayoweza kujitokeza ikiwemo upotevu wa
mali na makaazi yao.
akiwasilisha mada ya muelekeo wa mvua afisa mipango wa
kamisheni ya kukabiliana na maafa makame ali simai amesema juhudi za
kukabiliana na maafa zinahitaji mashirikiano kwa taasisi mbalimbali hivyo ni
vyema kwa wananchi kufuata sheria hususan katika ujenzi ili kuepuka kuziziba
njia za kupitisha maji ya mvua.
aidha ametowa wito kwa serikeli kuimarisha
miundombinu ya mitaro iliopo katika makaazi wananchi pamoja
na kuwachukulia hatua watu waliojenga nyumba za makaazi katika njia za
maji ya mvua ili kuyawezesha maji hayo kutotuama katika nyumba.
No comments