TUMBATU FM

Breaking News

Baraza la usalama kuhimiza hatua za pamoja ili kuboresha operesheni za ulinzi wa amani

Image result for Baraza la usalama images

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limechagua kauli mbiu yake kuu kwenye majadiliano ya wazi kwa mwezi huu kuwa ni "juhudi za pamoja kuboresha operesheni za ulinzi wa amani".

Mwenyekiti wa zamu na mwakilishi wa Uholanzi kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa Bw Karel van Oosterom, amesema pia kutakuwa na mikutano miwili inayohusiana na uhaba wa maliasili.

Baraza pia litakuwa na mikutano ya kawaida kuhusu masuala ya usalama ikiwa ni pamoja na ule unaohusu Afghanistan, ambao katika siku ya kimataifa ya wanawake utajadili mambo ya wanawake, amani na usalama nchini Afghanistan.

Na kuhusu mambo ya Afrika, baraza litakuwa na mikutano kadhaa kuhusu hali ya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na pia litaonageza mamlaka ya tume ya kulinda amani ya umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini.

No comments