Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limelaani mashambulizi kambi ya jeshi
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limelaani mashambulizi iliyoyaita ya kikatili na hofu kwenye kambi ya jeshi na ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu wa nchi ya Burkinafaso,Wagadugu ambapo katika shambulizi hilo la jana,watekelezaji wake wanane na maafisa wa usalama wanane waliuawa.
Baraza hilo limesema wale wote waliohusika katika shambulizi hilo lazima wapatikana na kufikishwa katika mkono wa sheria. Taarifa iliyotolewa na wizara ya mawasiliano ya nchi hiyo,imesema washambuliaji wanne waliuawa katika ofisi ya mkuu wa utumishi wa jeshi na wanne wengine waliuwa karibu na ubalozi wa Ufaransa. Serikali imesema kuwa idadi ya vifo haihusishi idadi ya raia waliouawa katika mashambulizi hayo.
wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Keneti Sawabogo,amekiambia kituo kimoja cha habari kuwa takribai watu 80 walijeruhiwa miongoni mwao hali zao zikiwa mbaya.
No comments