Waziri Mkuu Majaliwa Kassim aunga mkono FIFA mapambano ya rushwa
Rais wa FIFA Gianni Infantino akiwa Tanzania kwa ajili ya kongamano maalumu la kutathmini maendeleo ya mpira wa miguu (The Executive Football Summit) alipata fursa ya kukutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim.
Mh. Majaliwa ameupongeza uongozi wa FIFA kwa namna unavyosaidia maendeleo ya soka duniani.
“Tanzania inakupongeza sana kwa jitihada zinazolenga kuendeleza mpira wa miguu duniani kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa malengo ya kuendeleza mpira.”
“FIFA ikiwa ni kitovu cha mapambano dhidi ya rushwa, na sisi Tanzania tunaunga mkono kwa kuhakikisha kwamba sekta zote za michezo zinatumia vizuri rasilimali zilizopo kwa ajili ya kuendeleza michezo lakini pia tunasimamia vizuri matumizi sahihi ya madaraka katika sekta za michezo ili kuleta maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania.”
“Napenda kutamka kuwa tunaunga mkono jitihada hizi za FIFA CAF kwa mikono yetu miwili, ili kupata mafanikio makubwa katika mpira wa miguu hii ikiwa ni pamoja na kupata viongozi wenye muono wa mbali katika mpira wa miguu na mpango wa kuendeleza mpira wa miguu duniani kote.”
No comments