Rais wa FIFA kuhusu Mbwana Samatta
Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta anaipeperusha vilivyo bendera ya Tanzania, hiyo ni baada ya Rais wa FIFA Gianni Infantino kumtaja wakati akipiga stori mbili tatu na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
“Nilisikia mchezaji bora wa Afrika kutoka Tanzania Mbwana Samatta anacheza Genk, hii ni nchi ya mpira licha ya changamoto za shirikisho siku za nyuma lakini kwa sasa mpo kwenye mstari kutokana na uongozi mpya kwa kushirikiana na CAF pamoja na FIFA”-Gianni Infantino.
“Tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja kuleta maendeleo ya mpira, leo tumeileta dunia Dar es Salaam tuna wageni kutoka Asia, America ya Kaskazini, Carebean, Afrika na Fifa tupo hapa kwa hiyo ulimwengu upo hapa leo na nina furaha kwa hilo.”
Kama unakumbuka, Samatta alishinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Afrika) mwaka 2015 akiwa mchezaji wa TP Mazembe kabla hajajiunga na klabu ya Genk ya Ubelgiji anayoitumikia sasa.
No comments