Rais asisitiza jeshi la polisi kuendelea kufanya kazi zake vyema
Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la
mapinduzi dk. ali mohamed shein amesisitiza haja kwa jeshi la polisi kuendelea
kufanya kazi zake vyema hapa zanzibar
ili kuimarisha amani na utulivu iliyopo hasa ikizingatiwa kuwa uchumi wa
zanzibar unategemea utalii ambao unahitaji kuwepo kwa usalama.
Dk. shein ameyasema hayo leo ikulu mjini
zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na kamishna wa polisi zanzibar, mohamed
haji hassan aliyefika ikulu kwa ajili ya kujitambulisha akimuahidi kumpa mashirikiano makubwa kamishna huyo.
katika maelezo yake, dk. shein amemueleza
kamishna huyo mpya kuwa uchumi wa zanzibar unategemea kwa kiasi kikubwa katika
shuhuli za utalii, hivyo ni vyema usalama ukaimarishwa, ili sifa ya zanzibar
ikiunganishwa na vivutio vilivyopo izidi kuimarika na kuendelea kuwavutia
watalii kutoka pande zote za duniani.
Amemueleza kuwa mapato ya zanzibar yamezidi
kuongezeka sambamba na pato la taifa kutokana na kuongezeka kwa watalii kila
uchao na kupelekea kukua kwa uchumi wa zanzibar, ambapo hiyo yote inatokana na
kuwepo kwa usalama mkubwa kwa wananchi na wageni wanaokuja kuitembelea
zanzibar.
Hata hivyo dk. shein amesisitiza haja ya jeshi
hilo kuendeleza doria katika maeneo yote hapa nchini hasa katika ukanda wa
hoteli za kitalii sambamba na kuhakikisha watalii hawabughudhiwi na badala yake
wanapata huduma zote za kitalii zilizo nzuri na zenye usalama.
Aidha, amemueleza kamishna huyo mpya wa polisi
zanzibar haja ya kushirikiana vyema na jamii katika kupiga vita suala la
udhalilishji wa kijinsia kwa akina mama na watoto hasa ikizingatiwa kuwa jeshi
hilo ndio linaloshughulikia mashauri ya matukio hayo.
No comments